Rayvanny, Diamond Platnumz - Iyena lyrics

[Rayvanny, Diamond Platnumz - Iyena lyrics]

Hhhhmm! Ah! Leo Chereko chereko
Mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua
Ahsante mama ulinifunza nkajua
Baba kasema kuomba mwiko
Raha ya chumvi kununua tena si kwa nazi
Si hirizi za waganga
Kwa baraka za baba na mama tu na dua
Waambie paparazi pingamizi wenye viranga
Waliosema hayawi hayawi yamekuwa
O-o-o oh! Oh!

Iyena Iyena iyena Iyena
Iyena Iyena kwaheri tutaonana
Iyena Iyena (Aah ooh)
Iyena Iyena (Aah Iyeena) iyena Iyena
Ntawakumbuka sana

Ooh! Ndoa baraka ukipata ushukuru
Maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia niushinde ujana
Ili kesho mahususi kusudi wasinong'one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi nakuvisha waone
Wakale sumu wavimbe wapasuke

Eeh! Ati nashika nanga
Nteke nsichomoke ndani (Anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani
(Anameremeta) sio vijembe vya kanga
Waziwazi mambo hadharani (Anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani
(Anameremeta)

Iyena Iyena (Aah iyoyo)
Iyena Iyena (Aah Eeeh) iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (Oh! Kwaheri Baba Mama)
Iyena Iyena (Iyeeena) iyena Iyena (Aah Eeh)
Iyena Iyena ntawakumbuka sana

Imefika tamati tulisubiri kitambo
Leo samaki kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati yanavutia mapambo
Napata picha safi litanikoma bundle
Mwanamke usafi gaga kulisugua
Mume akirudi sharti viatu kumvua
Kitandani marashi massage kumchua
Kisha anza sayansi viuno kutengua
Mambo ya kuzima taa si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa mumeo aone shanga

Eeeeh! Makeup kinanda
Kaka suit kama mbunge (Anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje
(Anameremeta)
Momo ndani Shivo amekuja na Fumbwe
(Anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge
(Anameremeta)

Iyena Iyena (Aah iyeee)
Iyena Iyena (Aah iyoyo) iyena Iyena
Kwaheri tutaonana (Eh! Kwaheri Baba Mama)
Iyena Iyena (Iyeee) iyena Iyena (Hhhmm)
Iyena Iyena ntawakumbuka sana

Saa nataka kusasambua (Sasambu)
Me nasasambua (Sasambu)
Aby Dad nasasambua mimi (Sasambu) sasambua!
Tuone mguu moja juu (Sasambu)
Usishushe chini (Sasambu)
Cheza jitazame (Sasambu) sasambua!
Tuone aisha kimobitel (Sasambu)
Nipe za baloteli (Sasambu)
Nyonga kibaiskeli (Sasambu) sasambua!
Tuone akaa kama unashika ukuta (Sasambu)
Ifanye unashusha (Sasambu)
Taratibu zungusha (Sasambu) sasambua
Tuone sasambu! Sasambu! Sasambu!
Sasambua! Tuone
Kama unawasha bajaji (Sasambu)
Imwagie na maji (Sasambu)
Tuwakomeshe vizazi (Sasambu) sasambua!
Tuone

Interpretation for


Add Interpretation

Add extended interpretation

If you know what the artist is talking about, can read between the lines, and know the history of the song, you can add interpretation to the lyrics. After checking by our editors, we will add it as the official interpretation of the song!

Latest added interpretations to lyrics

A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z #
Interpret