Diamond Platnumz - Kosa Langu lyrics

Diamond Platnumz

Diamond Platnumz [Naseeb Abdul Juma Issack] Tandale, Dar es Salaam, Tanzania 🇹🇿

[Diamond Platnumz - Kosa Langu lyrics]

Ah! Barua yako uliyotuma kwa
Ricardo Momo nimeisoma
Ila nimechelewa kuijibu sababu
Moyoni imenchoma eeh!
Nliyo yategemea tofauti na nlicho kiona
Hata naandika hii barua
Huku roho yangu inansonona
Umesema nichane nguo
Pia funguo umeirudisha sawa
Simu niziweke kituo na sio chaguo
Nikome kabisa sawa
Umesema hata ile picha nzuri nliyo kukumbatia
Niichane sawa ila kinachoniumiza
Mbona moja umesahau

Kosa Langu Kosa Langu hujaniambia
Na kuniacha peke yangu ukanikimbia
Ila mbona kosa langu hujaniambia
Nami nikabiki peke yangu ukanikimbia

Aah! Mbona ukanichimbia kaburi


Ningari bado mzima niife nizikwe vizuri
Nipotee kabisa kimya licha ya matendo mazuri
Kwa upendo na heshima moto ukachochea tanuri
Ukachoma wangu mtimaa
Natamani hata ningepata nafasi
Muda wakati Kukutazama unione hata japo sura
Unitazame macho yangu
Mwenzako wimbi limenipiga kasi
Langu jahazi limezama mnyonge mwana Sanura
Wee ndio ulikuwa furaha yangu
Tatizo hata nkilia wa kunifuta machozi sina
Sawa na gari lisio na gear
La kuiforce ipande mlima
Ndio maana siishi kulalama
Japo jibu moja tuu linaloniumiza
Mwenzio bado sijaelewa

Kosa Langu Kosa Langu (Kosa Langu)
Hujaniambia (Hujaniambia)
Na kuniacha peke yangu (Peke yangu)
Ukanikimbia (Ukaenda)
Ila mbona Kosa Langu (Kosa Langu)
Hujaniambia (Hujaniambia Bado)
Nami nikabi peke yangu (Peke yangu)
Ukanikimbia (Ukaenda Ooh)

Oh moyo! Moyo wangu umevunjika una magongo
Oh moyo! Kila sehemu nayoshika kinyamazongo
Oh moyo!
Hata chozi likifutika linabaki tongo
Oh moyo!
Najitahidi kulidhika ila nna kinyongo
Oh moyo! Moyo wangu umevunjika Unaa jamani
Oh moyo! Hhhhmm hmm

Interpretation for


Add Interpretation

A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z #
Interpret