Diamond Platnumz, Prof. Jay - Kipi Sijasikia lyrics

[Diamond Platnumz, Prof. Jay - Kipi Sijasikia lyrics]

Ah niliacha kazi nifanye muziki
Wakatabiri nitalost
Wengine wakanishawishi tuloge kuondoa mikosi
Nakomaa na muziki ingawa jua la utosi
Naamini wote tunapita na
Kamwe maiti haijioshi
Jina langu lishatumika sana kutajirisha watu
Nyota ndogo alishasema kuna Watu na viatu
Bunduki haiui watu ila watu ndio wanaua watu
Dunia kama jalala tazama kwa Jicho la Tatu
Ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya
Tunawaita watakatifu kumbe ndio ma vampire
Yalisemwa mengi demu wangu alivyotoroka
Ni Fundisho tosha na
Changamoto kwa Mwanachoka
Nimepita Mengi mitihani ya kila Namna
Ndio maana mi sishangai
Wakiniita mbeba Lawama
Washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui
Wanadhani kila jogoo akiwikia ni Asubuhi
Riziki hamuwezi iziba labda
M'taichelewesha tuu
M'nakesha m'nishushe Mwenyezi ananipaisha
Kote milikobana kidume ndio Natusua
M'nanijua, Nakamua, roho za wangu zingaungua
Platnumz

Oh unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele
Nami nishike mkono nishinde
Unaehukumu ni wewe, ah
Mwenyezi Mungu naomba unilinde, ah
Kwenye hii vita milele
Mwanachoka dama nishinde

Walishazusha nimekufa eti nimepata ajali
Washindwe na walegee
Mwenyezi niepushie mbali
Wakasema nina Ukimwi kwa
Kuwa nilikonda ghafla
Wanataka kunizika mzima Kabla sijafa
Waliosema nina Ngoma wengine tushawafukia
Wanaomba nife leo naamini Watatangulia
Mama Pumzika Pema, Daima tunakulilia
Na bado wanachonga sana but man
The king is here
Daima m'taji wangu ni nguvu zangu mwenyewe
Simwamini m'tu kamwe naijamini mi mwenyewe
Hata nikinywa maji wanadai nakunywa pombe
Mi sijali i knock them hard, Mwana Lizombe
Bado tu napambana kibarua kisiote nyasi
Daima sitawadhuru wale wote walioniasi
Nikika kimya msidhani Sijasikia
Sio Bahati sio Ngekewa ni sauti Iliyobarikiwa
Holla

Oh unaehukumu ni wewe
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwenye hii vita milele
Nami nishike mkono nishinde
Unaehukumu ni wewe, ah
Mwenyezi Mungu naomba unilinde, ah
Kwenye hii vita milele
Mwanachoka dama nishinde

Mungu walaze pema Waliosemwa wakajiua
Ingawa wote tunapita naamini Maisha ni hatua
Maneno ya watu Sumu, yanaponya na Yanaua
Please nipe ujasiri mpaka siku Ukinichukua
Wape nguvu wale wote waliokata tamaa
Maneno yanaleta hila na Mzozo kwenye mitaa
Wanahesabu mabaya tuu na mema hawayaoni
Wanakuchekea Machoni, Wanakuroga Moyoni
Wanacheka chini chini wakati una Msiba
Wa kwanza kukutangaza kwa watu ukiwa na Shida
Wanatamani wapangue kila mola alichopanga
Wanatangaza Amani huku wameficha mapanga

(Eiih) Oh unaehukumu ni wewe (oheh)
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
(oh, ni wewe baba)
Kwenye hii vita milele (eh)
Nami nishike mkono nishinde
(oh, ni wewe baba) unaehukumu ni wewe, ah
Mwenyezi Mungu naomba unilinde, ah
(oh, ni wewe) kwenye hii vita milele
Mwanachoka dama nishinde

Tai mi maneno nishazoea (uh huh)
Ndio maana sijali wanapo ongea (uh huh) eih
Wanasemasema mengi, mengi, mengi
Tu hili mabaya (uh huh)
Oh, mi nimeshazoea (uh huh)
Ndio maana sijali wanapo ongea (uh huh) hey
Wanasemasema mengi, mengi, mengi

Iye, iye oh hey yeah
Oh yeah, yeah oh hey yeah
Iye, iye tuturururu
Tuturururu, yeah tuturururu, eh heh
Eh heh eh heh
Eh heh eh heh

Interpretation for


Add Interpretation

Add extended interpretation

If you know what the artist is talking about, can read between the lines, and know the history of the song, you can add interpretation to the lyrics. After checking by our editors, we will add it as the official interpretation of the song!

Latest added interpretations to lyrics

A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z #
Interpret